Gør som tusindvis af andre bogelskere
Tilmeld dig nyhedsbrevet og få gode tilbud og inspiration til din næste læsning.
Ved tilmelding accepterer du vores persondatapolitik.Du kan altid afmelde dig igen.
Kitabu hiki cha kiongozi cha mwalimu, kimekusudia kuwa mwongozo kwa ajili ya kuwafundisha wageni. Kitabu kinamwelekeza mwalimu namna ya kumfundisha mwanafunzi wa kiwango cha kwanza, cha pili, na cha tatu. Katika kila hatua ya kumfundisha mwanafunzi lugha ya Kiswahili, kumetumika mbinu mahsusi ili kuhakikisha mwanafunzi anafunzwa kwa umahiri mkubwa na anapata stadi ya kimawasiliano ya lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki ni muhimu kwa mtu yeyote anayetaka kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni.
Kitabu hiki cha Uandishi katika Kiswahili kinamwelimisha mwanafunzi wa uandishi namna bora ya kuandika kazi yake. Kazi mbalimbali za kiutungaji zimegusiwa ikiwa ni pamoja na insha, hotuba, risala, na utungaji. Mwandishi anaelezea hatua mbalimbali za kutunga insha na kuwasilisha mawazo yako kimantiki ili msomaji aelewe kinachosemwa na mwandishi. Vilevile amegusia aina za makala na sifa bainifu ya kuzitofautisha. Kuna makala za hoja, uelezaji, ufafanuzi, ushawishi na usimuliaji. Aina mbalimbali za makosa ya kawaida ya ujengaji hoja yanagusiwa pamoja na mapendekezo ya namna ya kuyaepuka. Mbali na kazi hizo, kitabu hiki pia kinaelezea matumizi sahihi ya alama za uandishi na uakifishi. Hivyo, hiki ni kitabu kizuri kitakachokusaidia kukuza stadi yako ya uandishi.
Tilmeld dig nyhedsbrevet og få gode tilbud og inspiration til din næste læsning.
Ved tilmelding accepterer du vores persondatapolitik.