Markedets billigste bøger
Levering: 1 - 2 hverdage

Bøger af Kalisti Mjuni

Filter
Filter
Sorter efterSorter Populære
  • af Kalisti Mjuni
    115,95 kr.

    "Mambo 15 Tunayokosea Wakati wa Kuomba", ni kitabu kinachoeleza makosa ambayo tumekuwa tukiyafanya wakati wa kuomba yanayosababisha maombi yetu yasijibiwe na Mungu Baba. Pia, kinaeleza utofauti uliopo kati ya sala na maombi; na kina shuhuda za kweli za watu waliojibiwa maombi yao kwa kutumia mbinu ambazo Mungu Baba anataka tuzitumie wakati wa kuomba.Hakuna mtu asiyekuwa na mahitaji ya kumuomba Mungu katika maisha yake. Tunaweza kudhani kwamba: watu wenye mali nyingi, kazi nzuri, elimu kubwa, vyeo au nyadhifa fulani; hawana shida katika maisha yao. Lakini ukweli ni kwamba, kila mtu ana shida au matatizo ambayo amekuwa akimuomba Mungu amuepushe nayo. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba: kwa nini maombi yetu yanachelewa kujibiwa au hayajibiwi kabisa na Mungu Baba? Majibu ya maswali hayo utayapata ndani ya kitabu hiki kupitia siri zilizojificha katika Maandiko Matakatifu.

Gør som tusindvis af andre bogelskere

Tilmeld dig nyhedsbrevet og få gode tilbud og inspiration til din næste læsning.