Markedets billigste bøger
Levering: 1 - 2 hverdage

Bøger af Mohammed Khelef Ghassani

Filter
Filter
Sorter efterSorter Populære
  • af Mohammed Khelef Ghassani
    98,95 kr.

    MUHTASARI WA KITABU: Andamo ni diwani ya tungo za ushairi zilizoandikwa na Mohammed Ghassani kwa muongo mmoja kuanzia miaka ya mwanzoni ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Ni tungo zinazoogelea pamoja naye kwenye bahari ya uzoefu wa mwanzo wa ujana kuelezea hadithi yake ya maisha, mtazamo wake juu ya yale yaliyokuwa yakitokea mbele ya macho yake na ufahamu wake kwa ulimwengu. Aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Fasihi na Utamaduni ya Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Bwana Abbas Mdungi, wakati akikabidhi ripoti ya mswaada wa diwani hii mwezi Oktoba 2003, aliandika hivi: .."..Mshairi ameibuni kazi yake kwa ustadi mkubwa kama kwamba ni mweledi katika utunzi ilhali hii ndiyo kazi yake ya kwanza kabisa. Mitindo aliyotumia ni mingi na mizuri ambayo inatafautiana na wakati wengine kushabihiana....Kwenye lugha, ametumia lugha ya ushairi - nyoofu, nzuri na telezi... Maudhui, bila shaka, ameyatumia vizuri kuweza kuelimisha jamii akijikita kwenye masuala ya utamaduni, siasa na uchumi, ingawa utamaduni umekuwa sura kubwa zaidi.....Kwa kawaida, washairi wa Afrika huzikita dhamira zao katika migogoro ya kimapenzi, kindoa, kidini, kikazi, kinyonyaji, kidemokrasia, uongozi mbaya, umangimeza, njaa, umasikini na maradhi, naye kwa ujumla amefanikiwa sana katika hilo...." Kwa hivyo, ndani ya Andamo, sio tu muna mwangwi wa sauti ya kijana anayejaribu kuiwasilisha hadithi yake kwa hadhira kwa njia ya kishairi, lakini pia ishara ya kuibuka kwa kipaji cha aina yake kwenye uwanja wa fasihi ya Kiswahili.

  • af Mohammed Khelef Ghassani
    348,95 kr.

    Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kuitambulisha navo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: "Samaki hajijui kuwa amerowa!" Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote.¿¿¿¿¿Mohammed Ghassani alizaliwa kisiwani Pemba mwaka 1977, ambako alikulia na kusomea had alipohamia kisiwani Unguja kwa ajili ya masomo na maisha mwaka 1996 a mwaka 2010 akahamia nchini Ujerumani, ambako ndiko anakoishi na kufanya kazi

  • af Mohammed Khelef Ghassani
    263,95 kr.

Gør som tusindvis af andre bogelskere

Tilmeld dig nyhedsbrevet og få gode tilbud og inspiration til din næste læsning.